"

Albamu ya Video

HALI YA HEWA TANZANIA 30.07.2024

ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2 limetolewa kwa baadhi ya maeneo

Imewekwa: Jul 30, 2025

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO TAREHE: 29/07/2025.

TAHADHARI: VIPINDI VIFUPI VYA UPEPO MKALI UNAOZIDI KM 40 KWA SAA NA MAWIMBI MAKUBWA YANAYOZIDI MITA 2 VINATARAJIWA KWA BAAADHI YA MAENEO YA UKANDA WA PWANI YA KUSINI MWA BAHARI YA HINDI (MIKOA YA LINDI NA MTWARA). ANGALIZO: VIPINDI VIFUPI VYA UPEPO MKALI UNAOFIKIA KILOMITA 40 KWA SAA NA MAWIMBI MAKUBWA YANAYOFIKIA MITA 2 VINATARAJIWA KWA BAADHI YA MAENEO YA UKANDA WA PWANI YA KASKAZINI MWA BAHARI YA HINDI (MIKOA YA TANGA, DAR ES SALAAM NA PWANI (IKIJUMUISHA VISIWA VYA MAFIA) PAMOJA NA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA), UKANDA WA ZIWA VIKTORIA (MIKOA YA KAGERA, GEITA, MARA, MWANZA NA SIMIYU) NA UKANDA WA KUSINI MWA ZIWA TANGANYIKA (MIKOA YA KATAVI NA RUKWA).

Imewekwa: Jul 29, 2025

HALI YA HEWA TANZANIA

1. TAHADHARI ya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2, imetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba). 2. ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa ziwa Viktoria (mikoa ya Kagera, Geita, Mara, Mwanza na Simiyu), ukanda wa ziwa Nyasa (mikoa ya Ruvuma, Njombe na Mbeya), ukanda wa ziwa Rukwa na ukanda wa kusini mwa ziwa Tanganyika (mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe).

Imewekwa: Jul 28, 2025

HALI YA HEWA TANZANIA

1. TAHADHARI ya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2, imetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba). 2.ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa kusini mwa ziwa Tanganyika (mikoa ya Katavi na Rukwa).

Imewekwa: Jul 27, 2025

UTABIRI WA HALI YA HEWA LEO 25.07.2025

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kusini kwa Pwani ya kaskazini na kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya kusini.

Imewekwa: Jul 25, 2025

UTABIRI WA HALI YA HEWA TANZANIA

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kusini kwa Pwani ya kaskazini na kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya kusini. Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa kiasi.

Imewekwa: Jul 24, 2025