Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Ndiyo, Tanzania inaweza kupatwa na mawimbi ya Tsunami, hususan katika mwambao wa bahari ya Hindi.
Kulipuka kwa Volkano katika bahari kunaweza kusababisha Tsunami kutokana na kuhamishwa ghafla kiasi kikubwa cha maji ya bahari.
Maeneo ya bahari yenye mitetemo inayotokana na nyufa katika miamba ya sakafu ya bahari husababisha tetemeko la ardhi ambapo kiasi kikubwa cha maji huhamishwa ghafla na kuzalisha mawimbi makubwa baharini.
Tsunami ni mfululizo wa mawimbi makubwa yaliyo na nguvu kubwa yanayotokana na tetemeko la ardhi chini ya bahari kuhamisha ghafla kiasi kikubwa cha maji ya bahari. Jina la mawimbi haya yaani “Tsunami”linetokana na maneno ya Kijapani “tsu”na “nami”yenye maana ya “bahari”na “wimbi”
Tofauti katika klaimatolojia inatoa mabadiliko ya tabia anga katika vipindi vifupi kama vile mwezi, msimu au mwaka, kwa upande mwingine mabadiliko ya hali ya hewa yanahusisha kubadilika kwa wastani wa hali ya hewa ya muda mrefu katika kipindi cha muongo au zaidi.
Ni tabia anga iliyo nje ya kawaida katika hali ya hewa ikilinganishwa na wastani wa muda mrefu kwa kipindi kifupi na katika eneo husika.
Mabadiliko ya miaka mingi katika klaimatolojia ya hali ya anga katika eneo kunakotokana na kubadilika kwa asili au kwa sababu za shughuli za kibinadamu katika anga au ardhi.
Hali ya hewa ni tabia anga ya muda uliopo au muda mfupi ujao kuanzia masaa mawili(2) hadi siku thelathini (30) inayoelezea viwango vya hali joto, mvua au upepo katika eneo husika.
Klaimatolojia ni wastani wa hali ya tabia anga ya muda mrefu kuanzia miaka 30 na kuendelea katika eneo husika.