Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

ISO 9001:2015 Imethibitishwa Kutoa Huduma za Hali ya Hewa kwenye Usafiri wa Anga
Utabiri wa Hali ya Hewa.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imepewa jukumu la kutoa utabiri wa hali ya hewa ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nyakati tofauti ikihusisha utabiri wa hali ya hewa wa sasa (saa 0-2), wa muda mfupi sana (saa 2-12), wa muda mfupi (saa 12-72) , wa muda wa kati siku 3-10, wa muda mrefu kidogo (siku 10 hadi mwezi 1) na wa muda mrefu (mwezi 1 hadi miaka 2).

Mamlaka imepewa nguvu ya kipekee katika shughuli za utabiri wa hali ya hewa na utoaji wa tahadhari za hali mbaya ya hewa ikiwa ni pamoja na Tsunami kwa umma na kutoa huduma za usalama wa hali ya hewa katika anga, baharini, kilimo, mafuta na gesi, shughuli za utafutaji na uokoaji n.k katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Utabiri wa Hali ya Hewa.