Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) hutoa taarifa na ushauri ambao ni muhimu kwa mkulima na watumiaji wengine kwa ajili ya mipango mbalimbali ya kilimo, umwagiliaji/ nishati, muda sahihi wa matumizi ya viuatilifu, mbolea, ufugaji wa Wanyama na Samaki, n.k.
Jarida la hali ya hewa kilimo hutolewa kwa siku kumi kumi na musimu. Toleo Maalum la Jarida hili ambalo lina utabiri wa msimu huandaliwa na kusambazwa kwa watumiaji kabla ya kuanza kwa msimu wa Vuli (OND)
mwezi Septemba, mvua za Msimu (NDJFMA) mwezi Octoba, na Masika (MAM) mwezi Februari kila mwaka. Jarida la Hali ya Hewa Kilimo huchapishwa katika lugha ya taifa (Kiswahili) na Kingereza.
Jarida la hali ya hewa kilimo, mbali na kutoa taarifa za hali ya hewa iliyopita na inayotarajiwa vile vile hutoa ushauri kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ili wachukue hatua stahiki kutokana na hali ya hewa inayotarajiwa.
TMA pia hufanya shughuli za uangazi kwa ajili ya utafiti wa kilimo ikiwa ni pamoja na Vituo vya Utafiti wa Kilomo Tanzania (TARI) kupitia vituo maalum vya hali ya hewa kilimo (Hombolo, Tumbi, Ilonga, Kibaha, Naliendele, Mlingano, Lyamungu, Uyole, Mbimba, Kizimbani, Matangatuani, Igeri, na Ukiriguru).
Kwa maelezo zaidi kuhusu machapisho na taarifa za hali ya hewa kilimo; bofya: Majarida ya Hali ya Hewa Kilimo. Majarida haya husambazwa pia kwa Baruapepe, na kupitia mfumo wa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi SMS (FarmSMS) kwa huduma mahususi za hali ya hewa kilimo.
TMA pia hufanya shughuli za uangazi kwa ajili ya utafiti wa kilimo ikiwa ni pamoja na Vituo vya Utafiti wa Kilomo Tanzania (TARI) kupitia vituo maalum vya hali ya hewa kilimo (Hombolo, Tumbi, Ilonga, Kibaha, Naliendele, Mlingano, Lyamungu, Uyole, Mbimba, Kizimbani, Matangatuani, Igeri, na Ukiriguru).
Kwa maelezo zaidi kuhusu machapisho na taarifa za hali ya hewa kilimo; bofya: Majarida ya Hali ya Hewa Kilimo.
Majarida haya husambazwa pia kwa Baruapepe, na kupitia mfumo wa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi SMS (FarmSMS) kwa huduma mahususi za hali ya hewa kilimo.
Hali ya Hewa Kilimo

