- Mamlaka yaHali ya Hewa, Tanzania ni nini na kazi zake ni zipi?
- Kivipi TMA inashirikiana na wadau wengine hasa sekta ya Kilimo na Menejimenti za Afya? (Swali hili hujitokeza mara nyingi pindi tunapotoa tahadhari za mapema za hali mbaya ya hewa lakini pia phenomena kama za El Nino au Tsunami)
- Wakulima kutaka kujua mwenendo wa mvua (hasa katika kipindi cha msimu).
- Wadau kutaka kujua au kulalamika kuwa hawapati ushauri wa kisekta kutoka kwa maafisa ugani?
- Ni njia zipi Mamlaka hutumia katika kusambaza taarifa zake za utabiri wa hali ya hewa na changamoto zake? (Hapa mara nyingi wasikilizaji hulalamika kutokupata taarifa kwa wakati hasa ngazi za vijiji?
- Kwa nini mvua inaweza kunyesha eneo moja na isinyeshe eneo lingine lakini mkoa ni huo huo mmoja)
- Ni kwa kiwango gani tabiri za hali ya hewa ni sahihi? (Hii mara nyingi inatokana na baadhi wa watumiaji kutoamini taarifa za utabiri zinazotolewa na Mamlaka)
- Je, Mamlaka hufanya jitihada gani kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinawafikia watuamiaji kwa wakati?
- Mamlaka hutumia njia gani katika kujenga uelewa kwa watuamiaji wa taarifa za hali ya hewa (Hapa wakati mwingine waandishi huuliza kama Mamlaka ina mpango wa kuanzisha clubs endelevu katika shule mbalimbali, ili kuendelea kujenga uelewa)
- Mabadiliko ya tabianchi/hali ya hewa yanaathiri vipi mwenendo wa mvua nchini?

