Huduma Zetu
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inalo jukumu la kukusanya na kutunza takwimu za Hali ya Hewa zinazo kusanywa kutoka katika vituo vya Hali ya Hewa hapa nchini. Takwimu hizo kama vile: Kiasi cha mvua, joto, hali ya unyevunyevu angani, muda wa uwakaji jua kwa siku, kasi na mwelekeo wa upepo, uvukizi, upeo wa kuona, mionzi ya jua, mawingu na mgandamizo wa hewa
Takwimu na taarifa za hali ya hewa zinaweza kutumika kwa ufanisi ili kupunguza baadhi ya majanga makubwa kwa jamii hususan majanga yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa. Sambamba na taarifa hizo Mamlaka pia hutoa takwimu, taarifa za hali ya hewa na ushauri wa kitaalam kwa watumiaji mbalimbali wa kitaifa, kikanda na wa kimataifa
Kwa ujumla, takwimu za hali ya hewa hutumika sana kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya kiuchumi, viwanda na utafiti wa kisayansi.