10 Days Forecast
MUHTASARI WA MWENENDO WA MVUA KWA TAREHE 11-20 SEPTEMBA, 2026 NA MATARAJIO YA MVUA KWA TAREHE 21-30 SEPTEMBA, 2026
MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA TAREHE 21-30 SEPTEMBA, 2026.
Kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Vipindi vya mvua zinazoambatana na ngururumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro,Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vyaMvua vinatarajiwa katika maeneo machache.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Hali ya ukavu inatarajiwa.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Hali ya ukavu inatarajiwa.
Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Hali ya ukavu inatarajiwa.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Hali ya ukavu inatarajiwa.
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua

