Mamlaka ya Hali ya Hewa hutoa huduma za hali ya hewa kwa watumiaji wote wa Bahari na Maziwa Makuu. Huduma hizi zinatolewa kama ilivyoelekekezwa kwenye Sheria ya Mamlaka Na. 2 ya 2019 kwenye kifungu 5(1) na 2(i) &(j). Huduma hizo zimelenga kwenye sekta ya usafirishaji, uvuvi, huduma za bandari, utafutaji wa mafuta na gesi katika Bahari, n.k.
Mamlaka ina wajibu wa kutoa tahadhari na ushauri wakati wa matukio ya hali mbaya ya hewa. Tahadhari hizo na ushauri hutolewa kila yanapotarajiwa matukio ya, upepo mkali na mawimbi makubwa kwenye Maziwa na Bahari
Utoaji wa huduma za hali ya hewa kupitia ofisi za bandari
Mamlaka ya Hali ya Hewa imewafikia wateja wake kwa kuwasambazia taarifa za hali ya hewa kupitia ofisi zake zilizoko kwenye Bandari
Utabiri wa Hali ya Hewa Majini

