Dira na Dhamira


Dira ya Mamlaka ya Hali ya Hewa:

"Kuwa kitovu bora cha huduma za hali ya hewa kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii"

Dhima ya Mamlaka ya Hali ya Hewa:

"Kuhakikisha uwepo wa huduma bora na za uhakika za hali ya hewa, zinazokidhi matarajio ya wadau kupitia utoaji na udhibiti wa huduma za hali ya hewa kwa usalama na maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania"

Maadili Muhimu:

Katika kutekeleza Dhima na Dira, Mamlaka inaamini na kufuata misingi ya:-

  • Utendaji unaozingatia taaluma;
  • Uwazi na uwajibikaji;
  • Utendaji kazi unaozingatia hali tofauti za wadau;
  • Utoaji huduma bora na kwa wakati;
  • Matumizi bora ya rasilimali;
  • Ufanyaji kazi wa pamoja; na
  • Kumjali mteja.