Huduma Zetu
Mamlaka ya Hali ya Hewa inatoa huduma mahususi kwa ajili ya taasisi zinazojihusisha na uhifadhi wa raslimali maji kwa matumizi ya nyumbani, kilimo, umeme wa maji, ujenzi, utalii, shughuli za biashara, viwanda na burudani, sekta ya afya na mazingira. Mamlaka pia hukusanya, huchakata na huhifadhi takwimu na taarifa za hali ya hewa-maji; na kuhamasisha jamii juu kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mafuriko na mvua kubwa.
Taarifa zitolewazo na Mamlaka zinazohusu zinazohusu unyeshaji wa mvua ni muhimu katika kung’amua vipindi vya mvua kubwa na uwezekano wa kutokea mvua kubwa, taarifa hii ni muhimu kwa wahandisi katika sekta ya ujenzi.