Historia

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilianzishwa kwa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Na.2 ya mwaka 2019, kupitia Tangazo la Serikali GN 459 la Tarehe 14 Juni 2019. Ikiwa na jukumu la kuratibu, kudhibiti na kutoa huduma za hali ya hewa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mamlaka hii inatokana na ulio kuwa wakala wa hali ya hewa Tanzania ulionzishwa kwa sheria ya wakala (Executive Agency Act) sura Na. 245 marejeo ya Mwaka 2022. Kabla ya wakala wa hali ya hewa, huduma za hali ya hewa nchini zilikuwa zinatolewa na iliyokuwa idara ya hali ya hewa nchini (Directorate of Meteorology) ambayo ilianzishwa Mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa iliyo kuwa jumuiya ya Africa Mashariki, iklwa na jukumu la kufanya uangazi na kutoa taarifa za hali ya hewa nchini.Kabla ya Jumuiya ya Africa Mashariki, huduma za hali ya hewa nchini zilitolewa chini ya Taasisi ya hali ya hewa iliyokuwa chini ya wakoloni.

Aidha, Mamlaka inamiliki Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kilichopo Kigoma(www.nmtc.ac.tz).