Huduma Zetu

services images

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa utabiri wa hali ya hewa kwa vipindi mbalimbali. Kwa kawaida Utabiri huu hutolewa kwa saa 2-12 (kuzingatia mahitaji), saa 24, siku 5, siku 10, utabiri wa mwezi na utabiri wa msimu.

Mamlakaina wajibu wa kutoa tahadhari na ushauri wakati wa matukio ya hali mbaya ya hewa. Tahadhari hizo na ushauri hutolewa kila yanapotarajiwa matukio ya upungufu wa mvua, mvua kubwa, upepo mkali, mawimbi makubwa, na joto au baridi kali