Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

ISO 9001:2015 Imethibitishwa Kutoa Huduma za Hali ya Hewa kwenye Usafiri wa Anga

MKURUGENZI MKUU WA LATRA AFURAHISHWA NA NJIA ZA USAMBAZAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA

News Image

MKURUGENZI MKUU WA LATRA AFURAHISHWA NA NJIA ZA USAMBAZAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), CPA, Dkt. Habibu Suluo, alipongeza juhudi za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa wananchi kupitia njia mbalimbali za usambazaji, hususan Chaneli ya WhatsApp alizungumza hayo alipotembelea banda la TMA kupitia maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yaliyofanyika tarehe 18 -23 Juni 2026 katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

Dkt. Suluo alikuwa mmoja wa wadau aliyeunganishwa kwenye Chaneli ya WhatsApp ya Mamlaka baada ya kupokea elimu juu ya huduma zitolewazo na TMA, Aidha alikiri kwa kusema matumizi ya majukwaa ya kidigitali yameongeza upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa kwa wakati na kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi.