Habari
Imewekwa:
Sep, 11 2025
MVUA ZA VULI 2025: MVUA ZA WASTANI HADI CHINI YA WASTANI ZINATARAJIWA KATIKA MAENEO MENGI YA NCHI.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema Mvua zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Chini ya Wastani katika maeneo mengi na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko wa mvua usioridhisha hususan katika maeneo ya pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki.