Habari

Imewekwa: May, 26 2023

TMA YATOA UTABIRI WA JUNI HADI AGOSTI 2023

TMA YATOA UTABIRI WA JUNI HADI AGOSTI 2023

Dodoma, Tarehe 26/05/2023.

“Hali ya joto la bahari katika ukanda wa tropiki ya kati ya bahari ya Pasifiki inatarajiwa kuwa ya juu ya wastani, hali inayoashiria uwepo wa El Niño katika msimu wa Kipupwe 2023, hivyo kutarajiwa kusababisha mchango mdogo katika mwenendo wa mvua nchini hususan maeneo ya pwani”. Alisema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang’a Dkt. Chang’a.

Dkt. Chang’a alizungumza hayo wakati akitoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa msimu wa Kipupwe unaotarajiwa kuanza mwezi Juni hadi Agosti (JJA) 2023. Dkt. Changa aliongezea Kwa kawaida, kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti (JJA), hutawaliwa na hali ya ukavu, baridi na upepo wa Kusi katika maeneo mengi ya nchi.

Aidha, upepo unaotarajiwa kuvuma kutoka Kusini-Mashariki na Mashariki (Matlai) katika ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi unatarajiwa kuleta unyevunyevu kutoka Bahari ya Hindi na kusababisha vipindi vya mvua katika maeneo machache ya ukanda wa pwani.

Kupitia taarifa yake alieleza athari zinazoweza kujitokeza pamoja na kutoa ushauri kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku, nakushauri jamii kuchukua tahadhari za kiafya dhidi magonjwa yanayoweza kusababishwa na baridi, vumbi na matumizi ya maji yasiyo safi na salama, huku wakulima wakihamasihswa kulima mbogamboga na mazao ya mizizi.