Habari

Imewekwa: Nov, 22 2024

TMA YAELEZA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWENYE KILIMO CHA MWANI

TMA YAELEZA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWENYE KILIMO CHA MWANI

Baku,Azerbaijan; Tarehe 22 Novemba, 2024; Kaimu Mkurugenzi wa TMA, Zanzibar, Masoud Faki ameeleza namna kilimo cha mwani kinavyoweza kuathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi. Alisema hayo wakati akiwasilisha mada katika Banda la Tanzania, lililopo kwenye Mkutano wa 29 wa Nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29), unaofanyika Baku,Azerbaijan..

Alieleza kuwa kilimo cha mwani kinaathiriwa zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa hususani mvua nyingi,joto kali na upepo mkali. Aidha, alifafanua, TMA inatoa huduma za utabiri ikiwemo Msimu na utabiri wa hali mbaya ya hewa wa siku tano ambao huwezesha wakulima kufanya maamuzi sahihi kama vile uchaguzi wa eneo linafaa ili kukabiliana na hali ya mvua nyingi ambayo husababisha upungufu wa kiwango cha chumvi na hivyo kusababisha magonjwa; maamuzi mengine ni uvunaji wa zao hilo ili kukabiliana na upepo mkali unaoweza kuleta madhara ya mwani kukatika na kupotelea baharini.