Habari

Imewekwa: Nov, 17 2023

TMA NA TRCS WASAINI MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO YA UTOAJI ELIMU NA USAMBAZAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA.

TMA NA TRCS WASAINI MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO YA UTOAJI ELIMU NA USAMBAZAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA.

Dar es Salaam; Tarehe 13 Novemba, 2023;

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) wamesaini rasmi makubaliano ya mashirikiano ya utoaji wa elimu na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa jamii ili kuweza kuwafikia kwa usahihi na wakati. Mkataba huo wa mashirikiano ulisainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TMA na Makamu Mwenyekiti Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi (IPCC) Dkt. Ladislaus Chang’a, na Katibu Mkuu wa TRCS Bi. Lucia Pande, Dar es Salaam,Tarehe 13 Novemba, 2023.

“TMA na TRCS zimeendelea kuimarisha zaidi mashirikiano ya kiutendaji ili kuweka nguvu za pamoja katika kuokoa maisha ya watu na mali zao kutokana na majanga yanayotokana na hali mbaya ya hewa, ambayo yanaendelea kuongezeka kwa idadi na ukubwa wa matukio. Makubaliano haya ni moja ya utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa kukabiliana na madhara yatokanayo na athari za El Nino”. Alisema Dkt. Chang’a.

Katika hatua nyingine, Bi. Lucia Pande alifafanua kuwa TMA na TRCS wamekuwa wakifanya kazi kwa pamoja kwa kipindi kirefu, hivyo katika hatua za kongeza ufanisi wa utendaji kazi wa pande zote mbili, wamefikia makubaliano ya pamoja ya kuweka ushirikiano kimaandishi. Hatua hii ni uhimu sana kwa TRCS katika kuimarisha matumizi sahihi ya taarifa za kisayansi za hali ya hewa zinazotolewa na TMA katika kujiandaa na kuchukua hatua stahiki wakati wa majanga.