Habari

Imewekwa: Aug, 21 2021

NMTC NA NIT KUONGEZA USHIRIKIANO WA ELIMU

NMTC NA NIT KUONGEZA USHIRIKIANO WA ELIMU

Dar es Salaam, 19 Agosti, 2021:

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa (NMTC), Ndg. Peter Mlonganile pamoja na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa wamesaini mkataba wa makubaliano (MoU) yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NIT jijini Dar es Salaam, tarehe 19/08/2021.

Lengo la makubaliano hayo ni kuongeza ushirikiano wa Elimu katika eneo la Tehama, pia kubadilishana na kupeana uzoefu kati ya wafanyakazi wa NMTC na NIT kwa maendeleo ya kiuchumi wa Taifa na watu.