Habari

Imewekwa: Jun, 03 2024

DKT.BITEKO AIPONGEZA TMA KWA KUTOA HUDUMA BORA ZA UTABIRI WA HALI YA HEWA

DKT.BITEKO AIPONGEZA TMA KWA KUTOA HUDUMA BORA ZA UTABIRI WA HALI YA HEWA

Dodoma; Tarehe 3 Juni, 2024;

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Dkt. Doto Biteko ameipongeza Mamalaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa kuendelea kutoa huduma bora za hali ya hewa nchini. Amesema hayo wakati alipotembelea banda la TMA kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani,yanayo fanyika katika viwanja vya JICC, mjini Dodoma.

Dkt.Biteko alikuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa Maadhimisho haya muhimu kwenye ukuaji wa sekta ya mazingira nchini na alitembelea Banda la TMA na kupokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dr Ladislaus Chang’a. “Hongereni sana kwa huduma bora za utabiri mnazitoa kila siku na zinatusaidia sana, hongereni sana” Alisema Dkt Biteko

Kwa upande wake Dkt Chang’a aliwaomba wananchi wa Dodoma na wale wa mikoa ya jirani watumie fursaha hii kwa kutembelea banda la TMA kwenye maadhimisho haya ili kujifunza maswala mbalimbali ya mazingira na masuala mbalimbali ya hali ya hewa , na huduma zitolewazo na TMA.

“Karibuni wananchi wote katika banda la TMA, mje kujifunza na kuongeza uelewa wa huduma za hali ya hewa na matumizi yake katika sekta zote za kiuchumi na kijamii. Kujifunza uhusiano wa hali ya hewa na mazingira yanayotuzunguka. Tunao wataalam bingwa wa hali ya hewa na wapo tayari kutoa elimu” Alisema Dkt. Chang’a

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inashiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya wiki ya Mazingira kwa mwaka 2024 yenye kauli Mbiu "urejeshwaji wa Ardhi, ustahimilivu wa hali ya Jangwa na ukame"