Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

ISO 9001:2015 Imethibitishwa Kutoa Huduma za Hali ya Hewa kwenye Usafiri wa Anga

Monthly Forecast

MUHTASARI WA HALI YA HEWA KWA MWEZI AGOSTI, 2026 NA MWELEKEO KWA MWEZI SEPTEMBA, 2026

Dondoo za tathmini ya Agosti, 2026 na mwelekeo wa Septemba, 2026:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Agosti, 2026 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto kwa mwezi Septemba, 2026 nchini.

 

  1. Katika kipindi cha mwezi Agosti, 2026 maeneo mengi  nchini yaliendelea kupata vipindi vya baridi ya wastani hadi baridi kali, hususan nyakati za usiku na asubuhi.
  2. Vipindi vya upepo mkali vilijitokeza katika baadhi ya maeneo katika kipindi cha mwezi Agosti 2026, hususan ukanda wa pwani, kanda ya kati pamoja na maziwa makuu. Aidha, vipindi vya mvua vilijitokeza katika maeneo machache ya mwambao wa pwani, ukanda wa ziwa Victoria na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki.
  3. Katika kipindi cha mwezi Septemba 2026 vipindi vya baridi ya vinatarajiwa kuendelea katika baadhi ya maeneo nchini. Aidha, vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya ukanda wa pwani, Ziwa Victoria, na nyanda za juu kaskazini mashariki. Vipindi vya upepo mkali vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo.

Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua