RAMADHANI OMARY ACHAGULIWA KATIBU WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA TMA

Mahali

MOROGORO

Tarehe

2023-04-03 - 2023-04-04

Muda

0900 - 1100

Madhumuni

HBAVGAXVXSS

Event Contents

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wamemchagua Ndg. Ramadhani Omary kuwa Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa TMA, kupitia kikao cha Baraza hili kinachoendelea Morogoro tarehe 03 na 04 Aprili 2023.

Ndg. Ramadhani Omary alichaguliwa kwa kupata kura 62 akifuatiwa na Katibu Msaidizi Bi. Mecklina Merchades kura 32, jumla ya kura zilizopigwa ni 94. Uchaguzi huo umesimamiwa na Bi. Christina Matega, Afisa kazi kutoka Wizara ya Kazi na Ajira, Morogoro.

Katika hatua nyingine, Baraza hilo lilitambulisha wimbo wa TUGHE-Taifa na kuzinduarasmi kipeperushi maalumu na bango la TUGHE-TMA ambavyo vitatumika katikakuitangaza TUGHE-TMA kwenye majukwaa mbalimbali kupitia dhana ya uzalendo, ubunifuna uwajibakaji.

Ndg. Ramadhani Omaryni Mchambuzi wa Hali ya Hewa kutoka Ofisi ya Kituo Kikuu cha Utabiri, dawati la utabiri wa muda mrefu, anachukua nafasi ya Ndg. Chuki Sangalugembe aliyemaliza muda wake kwa mujibu wa mkataba wa Baraza la Wafanyakazi wa TMA.

Washiriki

TMA STAFF

Ada ya Tukio

20,000

Simu

0000000

Barua pepe

met@meteo.go.tz