Taarifa za Utabiri
Mvua na ngurumo vinatarajiwa katika maeneo machache maeneo ya mikoa inayozunguka Ziwa Victoria.
MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 01-10 OKTOBA, 2023
Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Mvua na ngurumo za radi katika maeneo machache zinatarajiwa.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla, hata hivyo maeneo machache yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua nyepesi.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaampamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Mvua katika maeneo machache zinatarajiwa.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Mvua na ngurumo za radi zinatarajiwa katika maeneo machache.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Vipindi vya ukavu vinatarajiwa.
Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Vipindi vya ukavu vinatarajiwa.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Vipindi vya ukavu vinatarajiwa.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Vipindi vya ukavu vinatarajiwa.
Imetolewa na;
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Dondoo za tathmini ya Septemba, 2023 na mwelekeo wa Oktoba, 2023:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Septemba, 2023 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, 2023 nchini.
i. Katika kipindi cha mwezi Septemba, 2023 hali ya ukavu iliendelea kujitokeza katika maeneo mengi nchini. Hata hivyo, vipindi vichache vya mvua vilijitokeza katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani, nyanda za juu kaskazini mashariki, ukanda wa ziwa Victoria na maeneo ya magharibi mwa nchi. Aidha, vipindi vya baridi vilijitokeza katika maeneo machache hususani nyanda za juu kusini magharibi.
ii. Katika kipindi cha mwezi Oktoba 2023, mvua za Vuli zinatarajiwa kuanza katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Aidha, ongezeko kidogo la joto linatarajiwa katika baadhi ya maeneo nchini.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali pakua
Dondoo muhimu za msimu wa mvua za Vuli; Oktoba - Disemba 2023 Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli katika kipindi cha Oktoba – Disemba, 2023, ushauri kwa wadau wa sekta na mamlaka mbalimbali kama vile Kilimo na Usalama wa Chakula, Mifugo na Uvuvi, Utalii na Wanyamapori, Uchukuzi, Mamlaka za miji, Nishati, Maji na Madini, Afya pamoja na Menejimenti za Maafa. Baadhi ya mambo muhimu katika taarifa hii ni: - i. Uwepo wa El-Niño unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mvua za msimu wa Vuli, 2023. ii. Mvua za Vuli, 2023 zinatarajiwa kuwa za Juu ya Wastani hadi Wastani katika maeneo mengi ya pwani ya kaskazini na ukanda wa Ziwa Victoria. Aidha, kwa maeneo ya nyanda za Juu kaskazini mashariki na maeneo machache ya mashariki mwa Ziwa Victoria mvua zinatarajiwa kuwa za Wastani hadi Juu ya Wastani. iii. Mvua za Vuli, zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2023 katika maeneo ya magharibi mwa Ziwa Victoria na kusambaa katika maeneo mengine mwezi Oktoba, 2023. Kwa kawaida mvua za Vuli huisha mwezi Disemba, hata hivyo msimu huu mvua za nje ya msimu zinatarajiwa kuendelea Januari, 2024. iv. Ongezeko la mvua linatarajiwa katika kipindi cha mwezi Disemba, 2023. Athari zinazotarajiwa: i. Shughuli za kilimo zinatarajiwa kuendelea kama ilivyo kawaida kwa msimu wa Vuli, 2023. Hata hivyo, ongezeko la unyevu wa udongo linaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na shughuli za kilimo. ii. Kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka. iii. Magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na uchafuzi wa maji. |
Dar es Salaam |
|||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Tarehe | Hali ya Mchana | Kiwango cha Juu cha Joto | Kiwango cha Chini cha Joto | Mawio ya Jua | Machweo ya Jua | ||
02/10/2023 |
![]() Vipindi vya Jua |
31°C | 22°C | 06:08 | 18:17 | ||
02/10/2023 |
![]() Vipindi vya Jua |
31°C | 22°C | 06:08 | 18:17 | ||
03/10/2023 |
![]() Vipindi vya Jua |
31°C | 21°C | 06:08 | 18:17 | ||
02/10/2023 |
![]() Vipindi vya Jua |
31°C | 22°C | 06:08 | 18:17 | ||
03/10/2023 |
![]() Mvua Nyepesi |
31°C | 21°C | 06:08 | 18:17 |