Taarifa za Utabiri
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kutoka Kusini kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani yote; Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi makubwa kiasi.
MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 01-10 JUNI ,2025
Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Vipindi vya mvua zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Vipindi vya mvua nyepesi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani naDar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi upepo mkali na mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Vipindi vya mvua zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache hususan ya mkoa wa Kigoma.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Hali ya ukavu inatarajiwa.
Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Vipindi upepo mkali na mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.
Kwa maelezo zaidi tafadhali pakua...
Dondoo za tathmini ya Mei, 2025 na mwelekeo wa Juni, 2025:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Mei, 2025 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto kwa mwezi Juni, 2025 nchini.
- Katika kipindi cha mwezi Mei, 2025 vipindi vya mvua viliendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini, hususan yanayopata misimu miwili ya mvua, sambamba na vipindi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo.
- Kwa mwezi Juni 2025, hali ya joto la chini inatarajiwa kupungua katika maeneo mengi ya nchi ikiashiria kuanza kwa msimu wa Kipupwe (Juni-Agosti), 2025. Aidha, vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya mwambao wa pwani, ukanda wa Ziwa Victoria, na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki na kusini magharibi.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali pakua
Dondoo muhimu za hali ya hewa kipindi cha Juni-Agosti (JJA), 2025
Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa hali ya joto, upepo na mvua katika msimu wa Juni hadi Agosti (JJA), 2025; Ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao. Kwa kawaida, kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti (JJA), hutawaliwa na hali ya baridi na upepo mkali kwa maeneo mengi ya nchi. Kwa muhtasari, mwelekeo wa msimu wa JJA, 2025 unaonesha kuwa:
a) Mwelekeo wa hali ya joto
i. Hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi. Hata hivyo, hali ya baridi ya wastani hadi baridi kali inatarajiwa katika maeneo ya mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Singida pamoja na maeneo ya magharibi mwa mkoa wa Dodoma.
ii.Vipindi vya baridi zaidi vinatarajiwa kujitokeza katika mwezi Julai.
iii.Vipindi vya mvua za nje ya msimu vinatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria, ukanda wa mwambao wa pwani pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
b) Mwelekeo wa hali ya upepo
i. Msimu wa Kipupwe 2025 unatarajiwa kutawaliwa na upepo wa wastani utakaovuma kutoka Kusini Mashariki kwa maeneo mengi ya nchi, na vipindi vichache vya upepo mkali utakaovuma kutoka kusini (upepo wa kusi) hususan katika kipindi cha miezi ya Juni na Julai 2025 katika maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi na maeneo ya nchi kavu.
c) Athari
i. Magonjwa yanayohusiana na hali ya hewa ya baridi kama vile homa ya mapafu na magonjwa ya mifugo yanaweza kujitokeza, ingawa kwa kiasi kidogo.
ii. Hali ya vumbi linalosababishwa na upepo katika baadhi ya maeneo linaweza kupelekea uwepo wa magonjwa ya macho.
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua
Dar es Salaam |
|||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Tarehe | Hali ya Mchana | Kiwango cha Juu cha Joto | Kiwango cha Chini cha Joto | Mawio ya Jua | Machweo ya Jua | ||
01/06/2025 |
![]() Mvua |
28°C | 23°C | 06:27 | 18:11 | ||
01/06/2025 |
![]() Mvua |
29°C | 23°C | 06:30 | 18:11 | ||
02/06/2025 |
![]() Mvua |
29°C | 23°C | 06:30 | 18:11 | ||
01/06/2025 |
![]() Mvua |
30°C | 23°C | 06:30 | 18:11 | ||
02/06/2025 |
![]() Mvua Nyepesi |
29°C | 23°C | 06:30 | 18:11 |