Taarifa za Utabiri
- NGURUMO ZA RADI ZINATARAJIWA KATIKA MIKOA YA KAGERA NA MARA.
MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 11-20 SEPTEMBA, 2024
Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Mvua na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaampamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Mvua nyepesi zinatarajiwa katika maeneo machache.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Hali ya ukavu inatarajiwa.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Hali ya ukavu inatarajiwa.
Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Hali ya ukavu inatarajiwa.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Mvua nyepesi zinatarajiwa katika maeneo machache.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro: Hali ya ukavu inatarajiwa.
Imetolewa na;
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Agosti, 2024 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto kwa mwezi Septemba, 2024 nchini.
i. Katika kipindi cha mwezi Agosti, 2024 vipindi vya baridi hadi baridi kali viliendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini hususan yale yaliyopo nyanda za juu kusini magharibi na nyanda za juu kaskazini mashariki hasa nyakati za usiku na asubuhi.
ii. Vipindi vya upepo mkali vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini, hususan ukanda wa Pwani na maziwa makuu. Kwa upande mwingine, vipindi vichache vya mvua vilijitokeza katika ukanda wa Pwani, kanda ya Ziwa Victoria na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki.
iii. Katika kipindi cha mwezi Septemba 2024, hali ya ukavu inatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi nchini pamoja na ongezeko kiasi la joto katika baadhi ya maeneo. Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya mwambao wa pwani, ukanda wa Ziwa Victoria na maeneo yenye miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki. Aidha, vipindi vya upepo mkali vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo nchini katika hiki cha Septemba, 2024.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali pakua
Dondoo muhimu za msimu wa mvua za Vuli kipindi cha Oktoba – Disemba, 2024
Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli kipindi cha Oktoba - Disemba 2024, ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na uvuvi, maliasili, wanyamapori na utalii, nishati na maji, usafirishaji (nchi kavu, kwenye maji na angani), mamlaka za miji, afya pamoja na menejimenti za maafa. Utabiri huu ni mahsusi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (Nyanda za juu kaskazini mashariki, Pwani ya kaskazini, Ukanda wa Ziwa Viktoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma). Kwa muhtasari, mwelekeo huo na athari zake unaonesha kuwa:
a) Mvua za Vuli, 2024
i. Mvua zinatarajiwa kuwa za Chini ya Wastani hadi Wastani katika maeneo mengi na zinatarajiwa kuanza kwa kusuasua na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko wa mvua usioridhisha.
ii. Mvua za Vuli zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2024 katika ukanda wa Ziwa Victoria na kusambaa katika maeneo mengine katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Oktoba, 2024. Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya nne ya mwezi Disemba, 2024.
iii. Mvua za Vuli zinatarajiwa kuongezeka kidogo mwezi Disemba, 2024.
iv. Vipindi vya joto kali kuliko kawaida vinatarajiwa katika msimu wa Vuli.
v. Uwepo wa La-Niña hafifu unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mvua za msimu wa Vuli, 2024.
b) Athari zinazotarajiwa
i. Upungufu wa unyevunyevu katika udongo unatarajiwa kujitokeza katika maeneo mengi na hivyo kuathiri shughuli za kilimo.
ii. Kina cha maji katika mito na mabwawa vinatarajiwa kupungua.
iii. Kujitokeza kwa magonjwa ya mlipuko, kutokana na upungufu wa maji safi na salama.
Dar es Salaam |
|||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Tarehe | Hali ya Mchana | Kiwango cha Juu cha Joto | Kiwango cha Chini cha Joto | Mawio ya Jua | Machweo ya Jua | ||
11/09/2024 |
Vipindi vya Jua |
30°C | 22°C | 06:19 | 18:20 | ||
11/09/2024 |
Vipindi vya Jua |
28°C | 16°C | 06:30 | 18:31 | ||
12/09/2024 |
Vipindi vya Jua |
33°C | 19°C | 06:40 | 18:43 | ||
11/09/2024 |
Vipindi vya Jua |
28°C | 16°C | 06:30 | 18:31 | ||
12/09/2024 |
Vipindi vya Jua |
33°C | 19°C | 06:40 | 18:43 |