Taarifa za Utabiri
Mvua na ngurumo kwa maeneo machache...
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua......
MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 21-31 MACHI, 2023.
Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Mvua na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa katika maeneo machache.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Mvua na ngurumo za radi vinatarajiwa.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Mvua na ngurumo za radi vinatarajiwa kwa baadhi ya maeneo.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa.
Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Mvua na ngurumo za radi katika baadhi ya maeneo zinatarajiwa.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Mvua na ngurumo za radi vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Mvua na ngurumo za radi vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo.
Imetolewa na;
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Februari, 2023 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Machi, 2023 nchini.
- Kipindi cha mwezi Februari 2023, ongezeko la mvua lilijitokeza katika baadhi ya maeneo hususan wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi na kufuatiwa na upungufu wa mvua katika maeneo mengi ya nchi.
- Katika mwezi Machi 2023, vipindi vya mvua vinatarajiwa kuendelea katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Hata hivyo, mvua za Masika zinatarajiwa kuanza kwa baadhi ya maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.
- Hali ya joto inatarajiwa kuendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo ya nchi hususan yale yanayotarajiwa kuwa na upungufu wa mvua.
Dondoo muhimu za msimu wa mvua za Masika; Machi - Mei 2023
Taarifa hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za Masika katika kipindi cha Machi – Mei, 2023, ushauri kwa wadau wa sekta na mamlaka mbalimbali kama vile Kilimo na Usalama wa Chakula, Mifugo na Uvuvi, Utalii na Wanyamapori, Uchukuzi, Mamlaka za miji, Nishati, Maji na Madini, Afya pamoja na Menejimenti za Maafa. Baadhi ya mambo muhimu katika taarifa hii ni: -
i.Mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka isipokuwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es salaam, Pwani (ikijumuisha Mafia), kaskazini mwa Morogoro pamoja na kisiwa cha Unguja ambapo mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa.
ii.Ongezeko la mvua linatarajiwa katika kipindi cha mwezi Mei 2023, hususan katika maeneo ya pwani ya kaskazini.
iii.Mvua za Masika zinatarajiwa kuanza mwezi Machi, katika maeneo mengi na zinatarajiwa kuisha katika wiki ya nne ya mwezi Mei 2023 katika maeneo mengi ingawa mwendelezo wa mvua za nje ya msimu unatarajiwa mwezi Juni 2023 katika maeneo machache ya ukanda wa pwani ya kaskazini.
Athari zinazotarajiwa:
i.Mvua chache na zenye mtawanyiko usioridhisha katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani zinaweza kusababisha upungufu wa unyevu kwenye udongo na upatikanaji wa maji kwa ajili ya shughuli za kilimo.
ii.Katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani, unyevu wa udongo kupita kiasi unaweza kujitokeza na hivyo kuathiri ukuaji wa mazao ambayo hayahitaji maji mengi.
iii.Kwa kuwa maeneo mengi yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani, viwango vya maji katika mito na mabwawa havitarajiwi kuathirika zaidi.
Dar es Salaam |
|||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Tarehe | Hali ya Mchana | Kiwango cha Juu cha Joto | Kiwango cha Chini cha Joto | Mawio ya Jua | Machweo ya Jua | ||
23/03/2023 |
![]() Mvua na Ngurumo |
33°C | 27°C | 06:28 | 18:33 | ||
23/03/2023 |
![]() Mvua |
33°C | 27°C | 06:28 | 18:33 | ||
24/03/2023 |
![]() Mvua na Ngurumo |
32°C | 24°C | 06:28 | 18:33 | ||
23/03/2023 |
![]() Mvua na Ngurumo |
33°C | 24°C | 06:28 | 18:33 | ||
24/03/2023 |
![]() Mvua na Ngurumo |
33°C | 25°C | 06:28 | 18:33 |