Tahadhari Pakua
UPEPO MKALI NA MAWIMBI MAKUBWA.
1.TAHADHARI ya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2, imetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).
2. ANGALIZO la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa ziwa Viktoria (mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara na Simiyu) na ukanda wa kusini mwa ziwa Tanganyika (mikoa ya Katavi na Rukwa).