Huduma Zetu

services images

Chuo cha Taifa Cha Hali ya Hewa kinatoa Programu zifuatazo;

Astashahada ya Awali ya Hali ya Hewa (NTA LEVEL 4) ambayo inatambulika na Shirika la Hali ya Hewa Duniani kama ‘WMO-Meteorological Technician Entry-Level’. programu hii ni ya Mwaka mmoja yenye mihula miwili ikihusisha Jumla ya moduli kumi na moja (11).

Muhitimu wa programu hii anaweza kufanya kazi ya uangazi wa hali ya hewa,

Astashahada ya Hali ya Hewa (NTA LEVEL 5) ambayo inatambulika na Shirika la Hali ya Hewa Duniani kama ‘WMO-Meteorological Technician Mid-Level’. programu hii ni ya Mwaka mmoja yenye mihula miwili ikihusisha Jumla ya moduli kumi na mbili (12).

Muhitimu wa programu hii anaweza kufanya kazi ya uangazi wa hali ya hewa, aidha Muhitimu anatarajiwa kufanya kazi katika sekta mbalimbali kama vile Usafiri wa anga, Kilimo, Maji, Utalii, Ikolojia, Ulinzi na Usalama, Uvuvi, Viwanda, Ujenzi, Taasisi za Elimu na Utafiti,Usafiri wa Majini na nchi Kavu na Menejimenti ya Maafa.

Stashahada ya Hali ya Hewa (NTA LEVEL 6) ambayo inatambulika na Shirika la Hali ya Hewa Duniani kama ‘WMO-Meteorological Technician Senior Level’. programu hii ni ya Miaka miwili yenye mihula minne ikihusisha Jumla ya moduli ishirini na nane (28).

Muhitimu wa programu hii anaweza kufanya kazi ya Utabiri wa hali ya hewa, Kuchambua na kutafsiri Taarifa za hali ya hewa na kuzitumia kwenye sekta mbalimbali kama vile: Kilimo, Usafiri wa Anga na Majini na katika Tafiti za Hali ya Hewa na Menejimenti ya Mazingira.

Kwa maelezo zaidi kuhusianan na Chuo, tafadhali tembelea www.nmtc.ac.tz