Machapisho
UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI DESEMBA, 2025
PakuaDondoo za tathmini ya Novemba, 2025 na mwelekeo wa Desemba, 2025:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Novemba, 2025 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Desemba, 2025 nchini.
- Katika kipindi cha mwezi Novemba, 2025 vipindi vya mvua vilijitokeza katika maeneo machache nchini, hususan ukanda wa pwani, ukanda wa Ziwa Victoria na magharibi mwa nchi. Aidha, vipindi vichache vya mvua kubwa vilijitokeza.
- Katika kipindi cha mwezi Desemba 2025, mvua zinatarajiwa katika baadhi ya maeneo zikiwa na mtawanyiko usioridhisha. Aidha, vipindi vichache vya mvua kubwa vinatarajiwa katika maeneo machache.
- Hali ya joto inatarajiwa kuendelea katika maeneo yanayotarajiwa kuwa na upungufu wa mvua.
