Machapisho

TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI SEPTEMBA NA OKTOBA, 2025

Pakua

Katika kipindi cha mwezi Septemba 2025 hali ya ukavu iliendelea kujitokeza katika maeneo mengi ya nchi ikiambatana na hali ya joto nyakati za mchana. Aidha, mwezi Oktoba, 2025 vipindi vya mvua vilijitokeza katika maeneo machache na kuashiria kuanza kwa msimu wa mvua za Vuli, hususan ukanda wa ziwa Victoria. Aidha, mtawanyiko wa mvua hizo haukuwa wa kuridhisha katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Hali hii ilisababisha ongezeko kidogo la unyevu ardhini, kina cha maji na malisho kwa maeneo machache.

Hata hivyo, vipindi vifupi vya upepo mkali vilijitokeza katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani, kati mwa nchi, nyanda za juu kusini magharibi na maeneo ya maziwa makuu.

Hali ya hewa iliyojitokeza pamoja na athari zake imeendana na taarifa ya mwelekeo wa mvua za Vuli (Oktoba-Disemba), 2025.