Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI NOVEMBA, 2025

Pakua

Dondoo za tathmini ya Oktoba, 2025 na mwelekeo wa Novemba, 2025:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, 2025 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Novemba, 2025 nchini.

i. Katika kipindi cha mwezi Oktoba, 2025 vipindi vya mvua vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini, hususan yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka ikiashiria kuanza kwa mvua za Vuli, 2025 katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria. Aidha, vipindi vichache vya mvua kubwa vilijitokeza.

ii. Katika kipindi cha mwezi Novemba 2025, mvua za Msimu zinatarajiwa kuanza katika baadhi ya maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Aidha, mvua za Vuli zinatarajiwa kuanza katika maeneo ya ukanda wa pwani ya kaskazini na nyanda za juu kaskazini mashariki.

iii. Hali ya joto inatarajiwa kuendelea katika maeneo yanayotarajiwa kuwa na upungufu wa mvua.