Machapisho
MATARAJIO YA MVUA KWA TAREHE 11-20 NOVEMBA, 2025
PakuaMWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 11-20 NOVEMBA, 2025
Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa katika maeneo machache.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache hasa katika nusu ya kwanza ya dekadi.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaampamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache hasa katika nusu ya kwanza ya dekadi.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa katika maeneo machache.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.
Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.
Imetolewa na:
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
