Machapisho

MUHTASARI WA HALI YA HEWA KWA MWEZI SEPTEMBA, 2025 NA MWELEKEO KWA MWEZI OKTOBA, 2025.

Pakua

Dondoo za tathmini ya Septemba, 2025 na mwelekeo wa Oktoba, 2025:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Septemba, 2025 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, 2025 nchini.

i.Katika kipindi cha mwezi Septemba, 2025 hali ya ukavu pamoja na vipindi vya baridi hususan katika nyakati za usiku vilijitokeza katika maeneo machache. Hata hivyo, vipindi vichache vya mvua vilijitokeza katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani, nyanda za juu kaskazini mashariki na ukanda wa ziwa Victoria.

ii.Katika kipindi cha mwezi Oktoba 2025, mvua za Vuli zinatarajiwa kuanza katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Aidha, mvua za chini ya wastani hadi wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi.

iii.Katika kipindi cha Oktoba, 2025, ongezeko kidogo la joto linatarajiwa katika baadhi ya maeneo.