Machapisho
MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA ZA VULI (OKTOBA – DESEMBA), 2025 KWA MKOA WA MWANZA
PakuaDondoo
(i).Kwa ujumla mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya mkoa wa Mwanza isipokuwa maeneo machache ya kaskazini magharibi mwa mkoa ambayo yanatarajiwa kupata mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani.
(ii).Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Oktoba, 2025.
(iii).Mvua zinatarajiwa kuisha mwezi Januari, 2026.
(iv).Vipindi virefu vya ukavu vya siku kumi (10) au zaidi vinatarajiwa katika msimu huu wa Vuli.
Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua.