Machapisho

TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI JULAI NA AGOSTI, 2025

Pakua

Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Agosti, 2025 vipindi vya ukavu pamoja na baridi ya wastani hadi baridi kali hususan nyakati za usiku na asubuhi iliendelea kujitokeza katika maeneo mengi nchini. Hali hii ilisababisha upungufu wa unyevu ardhini, kupungua kwa maji na malisho pamoja na kuwepo kwa hali vumbi. Hata hivyo, vipindi vya upepo mkali uliofikia au kuzidi kasi ya kilomita 40 kwa saa vilijitokeza katika baadhi ya maeneo, hususan maeneo ya ukanda wa pwani na maziwa makuu.

Ingawa hali ya ukavu imeendelea kujitokeza katika maeneo mengi ya nchi lakini vipindi vichache vya mvua vilijitokeza katika maeneo ya ukanda pwani, Ziwa Victoria na maeneo yenye miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki. Aidha, hali ya hewa iliyojitokeza pamoja na athari zake imeendana na taarifa ya mwelekeo wa msimu wa Kipupwe (Juni-Agosti), 2025 iliyotolewa mwezi Mei 2025.