Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI SEPTEMBA 2025

Pakua

Dondoo za tathmini ya Agosti, 2025 na mwelekeo wa Septemba, 2025:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Agosti, 2025 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto kwa mwezi Septemba, 2025 nchini.

  • Katika kipindi cha mwezi Agosti, 2025 hali ya baridi ilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini, hususani nyakati za usiku na asubuhi. Hali ya baridi zaidi ilijitokeza katika maeneo ya nyanda za juu kusini magharibi.
  • Vipindi vifupi vya mvua zilizoambatana na radi vilijitokeza katika maeneo machache ya Ziwa Victoria. Hata hivyo, ukanda wa pwani pamoja na nyanda za juu kaskazini mashariki vilipata vipindi vya mvua nyepesi katika maeneo machache. Aidha, vipindi vya upepo mkali unaofikia kasi ya kilometa 40 kwa saa vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini.
  • Kwa mwezi Septemba 2025, hali ya baridi inatarajiwa kuendelea katika baadhi ya maeneo nchini hususani katika maeneo ya nyanda za juu kusini magharibi ikiambatana na hali ya ukavu kwa ujumla. Aidha, vipindi vichache vya mvua vinatarajiwa katika maeneo ya mwambao wa pwani, ukanda wa Ziwa Victoria, na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki.