Machapisho
MATARAJIO YA MVUA KWA TAREHE 01-10 OKTOBA, 2025
PakuaMWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 01-10 OKTOBA, 2025
Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Vipindi vya mvua zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.
Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaampamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vya mvua nyepesi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Vipindi vya mvua zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache hususan katika nusu ya pili ya dekadi.
Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Hali ya ukavu inatarajiwa.
Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Hali ya ukavu inatarajiwa.
Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Vipindi vya mvua nyepesi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Vipindi vya mvua nyepesi vinatarajiwa katika maeneo machache.
Imetolewa na:
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA