Machapisho

MUHTASARI WA MWENENDO WA MVUA KWA TAREHE 01-10 AGOSTI, 2025

Pakua

MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 11-20 AGOSTI, 2025

Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Vipindi vya mvua zinazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.

Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.

Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaampamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vya mvua nyepesi vinatarajiwa katika maeneo machache.

Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Hali ya ukavu inatarajiwa.

Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Hali ya ukavu inatarajiwa.

Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Hali ya ukavu inatarajiwa.

Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.

Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Hali ya ukavu inatarajiwa.

Imetolewa na:

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA