Machapisho
UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI AGOSTI, 2025
PakuaDondoo za tathmini ya Julai, 2025 na mwelekeo wa Agosti, 2025:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Julai, 2025 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto kwa mwezi Agosti, 2025 nchini.
- Katika kipindi cha mwezi Julai, 2025 hali ya baridi ilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini, hususani nyakati za usiku na asubuhi. Hali ya baridi zaidi ilijitokeza katika maeneo ya nyanda za juu kusini magharibi.
- Vipindi vya mvua vilijitokeza katika maeneo machache ya ukanda wa pwani, Ziwa Victoria na nyanda za juu kaskazini mashariki, hususan katika wiki mbili za mwanzo za mwezi Julai 2025. Aidha, vipindi vya upepo mkali unaofikia kasi ya kilometa 40 hadi 50 kwa saa vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini.
- Kwa mwezi Agosti 2025, hali ya baridi inatarajiwa kuendelea katika baadhi ya maeneo nchini ikiambatana na hali ya ukavu. Aidha, vipindi vichache vya mvua vinatarajiwa katika maeneo ya mwambao wa pwani, ukanda wa Ziwa Victoria, na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki.