Machapisho
TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI MEI NA JUNI, 2025
PakuaKatika kipindi cha mwezi ya Mei, 2025 mvua ziliendelea katika baadhi ya maeneo nchini, sambamba na ongezeko kidogo la mvua katika hususan katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Hali hii ilisababisha ongezeko la unyevu ardhini, kina cha maji na malisho kwa baadhi ya maeneo. Aidha, lakini pia ilisababisha mafuriko na kutuama kwa maji katika maeneo mengine. Kwa mwezi Juni 2023 baadhi ya maeneo yalipata vipindi vya upepo mkali pamoja na hali ya baridi, ikiashiria kuanza kwa msimu wa Kipupwe 2025. Hali ya hewa iliyojitokeza pamoja na athari zake imeendana na taarifa za mwelekeo wa hali ya hewa za misimu zilizotolewa hapo awali.