Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI JULAI, 2025

Pakua

Dondoo za tathmini ya Juni, 2025 na mwelekeo wa Julai, 2025:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Juni, 2025 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa hususan hali ya joto kwa mwezi Julai, 2025 nchini.

  • Katika kipindi cha mwezi Juni, 2025 hali ya baridi ilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini, hususani nyakati za usiku na asubuhi.
  • Vipindi vya mvua viliendelea kujitokeza katika maeneo machache ya ukanda wa pwani, Ziwa Victoria na nyanda za juu kaskazini mashariki, hususan katika wiki mbili za mwanzo za mwezi Juni 2025. Aidha, vipindi vya upepo mkali unaofikia kasi ya kilometa 40 hadi 50 kwa saa vilijitokeza katika baadhi ya maeneo nchini.
  • Kwa mwezi Julai 2025, hali ya baridi inatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi ya nchi ikiambatana na hali ya ukavu. Aidha, vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya mwambao wa pwani, ukanda wa Ziwa Victoria, na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki na nyanda za juu kusini magharibi.