Machapisho

TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI MACHI NA APRILI, 2025

Pakua

Katika kipindi cha miezi ya Machi na Aprili, 2025 mvua ziliendelea katika maeneo mengi ya nchi sambamba na ongezeko kidogo la mvua katika baadhi ya maeneo. Hali hii ilisababisha ongezeko la unyevu ardhini, kina cha maji na malisho kwa baadhi ya maeneo, lakini pia mafuriko na kutuama kwa maji katika maeneo mengine. Hali ya joto nyakati za mchana ilijitokeza katika maeneo yaliyokuwa na upungufu wa mvua hususan yale yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka katika kipindi cha mwezi Machi na kuathiri shughuli zinazofanyika maeneo ya nje/wazi. Kwa upande mwingine, vipindi vya upepo mkali vilijitokeza katika maeneo ya ukanda wa Pwani, Ziwa Victoria na nyanda za juu kaskazini mashariki. Hali ya hewa iliyojitokeza pamoja na athari zake imeendana na taarifa za mwelekeo wa mvua za msimu zilizotolewa hapo awali.