Machapisho
UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI MEI, 2025
PakuaDondoo za tathmini ya Aprili, 2025 na mwelekeo wa Mei, 2025:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Aprili, 2025 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Mei, 2025 nchini.
- Katika kipindi cha mwezi Aprili, 2025 maeneo mengi ya nchi yaliendelea kupata vipindi vya mvua na ngurumo. Aidha, vipindi vya mvua kubwa vilijitokeza katika baadhi ya maeneo na kusababisha athari ikiwemo mafuriko na kutuama kwa maji.
- Katika kipindi cha mwezi Mei 2025, mvua za Masika zinatarajiwa kuendelea katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka. Vilevile, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa katika maeneo machache yapatayo msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Aidha, ongezeko la mvua linatarajiwa katika baadhi ya maeneo. Kwa upande mwingine, hali ya joto inatarajiwa kupungua kiasi katika baadhi ya maeneo.