Machapisho

MATARAJIO YA MVUA KWA TAREHE 21- 30 JUNI, 2025

Pakua

MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 21-30 JUNI, 2025

Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Vipindi vya mvua zinazoambatana na nguromo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.

Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Vipindi vya mvua nyepesi vinatarajiwa hususan katika sehemu zenye miinuko.

Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaampamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vya upepo mkali na mvua nyepesi vinatarajiwa katika maeneo machache.

Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.

Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Hali ya ukavu inatarajiwa.

Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.

Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Hali ya ukavu kwa ujumla na vipindi upepo mkali vinatarajiwa.

Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.

Imetolewa na;

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA