Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI APRILI, 2025

Pakua

Dondoo za tathmini ya Machi, 2025 na mwelekeo wa Aprili, 2025:

Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Machi, 2025 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Aprili, 2025 nchini.

  • Katika kipindi cha mwezi Machi, 2025 maeneo mengi ya nchi yalipata vipindi vya mvua zilizoambatana na ngurumo katika baadhi ya maeneo hususan kuanzia wiki ya pili ya mwezi. Aidha, vipindi vya mvua kubwa vilijitokeza katika baadhi ya maeneo na kusababisha athari ikiwemo mafuriko na kutuama kwa maji.
  • Katika kipindi cha mwezi Aprili 2025, mvua za msimu zinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi. Aidha, ongezeko la mvua linatarajiwa katika baadhi ya maeneo. Kwa upande mwingine, joto linatarajiwa kupungua kiasi katika baadhi ya maeneo.