Machapisho
TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI JANUARI NA FEBRUARI, 2025
PakuaKatika kipindi cha miezi ya Januari na Februari, 2025 vipindi vya mvua vilijitokeza katika maeneo mengi ya nchi sambamba na ongezeko kidogo la mvua katika maeneo ya kusini mwa nchi hususan mwezi February. Hali hii ilisababisha kuongezeka na kuimarika kwa hali la unyevu ardhini, kina cha maji na malisho kwa baadhi ya maeneo, lakini pia mafuriko na kutuama kwa maji katika maeneo mengine. Hali ya ongezeko la joto nyakati za mchana ilijitokeza katika maeneo yaliyokuwa na upungufu wa mvua hususan yale yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka katika kipindi cha mwezi Februari, na kuathiri shughuli zinazofanyika maeneo ya nje/wazi. Kwa upande mwingine, vipindi vya upepo mkali vilijitokeza katika maeneo machache ya ukanda wa pwani na nyanda za juu kusini magharibi. Hali ya hewa iliyojitokeza pamoja na athari zake imeendana na taarifa ya mwelekeo wa mvua za Msimu, 2024/2025 iliyotolewa hapo awali.