Machapisho

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA MWEZI MACHI, 2025

Pakua

Dondoo za tathmini ya Februari, 2025 na mwelekeo wa Machi, 2025:
Taarifa hii inatoa muhtasari wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na mwenendo wa hali ya hewa kwa mwezi Februari, 2025 na kutoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa mwezi Machi, 2025 nchini.

  • Katika kipindi cha mwezi Februari, 2025 vipindi vya ukavu pamoja na hali ya joto vilijitokeza katika maeneo mengi ya nchi hususan kuanzia wiki ya pili ya mwezi. Aidha, baadhi ya maeneo yalipata mvua pamoja ngurumo. Aidha, vipindi vya mvua kubwa vilijitokeza katika maeneo machache na kusababisha athari ikiwemo mafuriko na kutuama kwa maji.
  • Katika kipindi cha mwezi Machi 2025, mvua za Masika zinatarajiwa kuanza katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka, na mvua za Msimu zinatarajiwa kuendelea katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Aidha, ongezeko la mvua linatarajiwa katika maeneo machache.