Machapisho

MATARAJIO YA MVUA KWA TAREHE 01- 10 MACHI, 2025

Pakua

MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 01-10 MACHI, 2025

Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara):

Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.

Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.

Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaampamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Hali ya ukavu kwa ujumla inatarajiwa.

Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa katika katika maeneo machache ya mkoa wa Kigoma na hali ya ukavu kiujumla inatarajiwa katika maeneo ya mikoa Katavi na Tabora.

Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Mvua zinatarajiwa katika maeneo machache.

Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa katikabaadhi ya maeneo.

Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Mvua nyepesi zinatarajiwa katika maeneo machache.

Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa katika maeneo machache.

Imetolewa na;

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA