Machapisho

TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA KWA MWEZI NOVEMBA NA DESEMBA, 2024

Pakua

Katika kipindi cha mwezi Novemba na Desemba, 2024 vipindi vya mvua vilijitokeza katika maeneo mbalimbali nchini, huku ongezeko kidogo la mvua likijitokeza mwezi Desemba. Hali hii ilisababisha ongezeko kidogo la unyevu ardhini, kina cha maji na malisho katika baadhi ya maeneo, lakini pia ilipelekea mafuriko na kutuama kwa maji katika baadhi ya maeneo. Hali ya joto inayoathiri shughuli zinazofanyika nje hasa nyakati za mchana ilijitokeza hususan katika maeneo yaliyopata vipindi vichache vya mvua. Aidha, vipindi vya upepo mkali vilijitokeza katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani na nyanda za juu kusini magharibi. Hali ya hewa iliyojitokeza pamoja na athari zake imeendana na taarifa ya mwelekeo wa mvua za Msimu (Vuli, 2024 na Msimu 2024/2025) zilizotolewa awali.