Machapisho

MATARAJIO YA HALI YA HEWA KWA TAREHE 1 - 10 FEBRUARI, 2023.

Pakua

MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE (01 - 10 FEBRUARI, 2023).

Kanda ya ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Vipindi vya mvua na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.

Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro): Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache.

Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaampamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo katika maeneo machache vinatarajiwa.

Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Vipindi vya mvua na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.

Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Vipindi vichache vya mvua na ngurumo za radi katika maeneo machache vinatarajiwa.

Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Vipindi vya mvua na ngurumo za radi katika baadhi ya maeneo vinatarajiwa.

Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Vipindi vya mvua na ngurumo za radi katika maeneo machache vinatarajiwa.

Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Vipindi vya mvua na ngurumo za radi katika baadhi ya maeneo vinatarajiwa

Imetolewa na;

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA