Machapisho
MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA ZA MASIKA (MACHI – MEI), 2025 KWA MAENEO YA KASKAZINI MWA MKOA WA KIGOMA
Pakua(i)Kwa ujumla mvua za Wastani hadi Chini ya Wastani zinatarajiwa katika maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.
(ii)Mvua zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi, 2025.
(iii)Mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya kwanza ya mwezi Mei, 2025.
(iv)Upo uwezekano wa kutokea vipindi vya ukavu vya siku kumi (10) au zaidi katika msimu huu wa Masika, 2025.